Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Kumbe Tambwe Alikuwa Na Kesi Mahakamani Huko Kwao Burundi

Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Tambwe anatarajia kurejea nchini kesho baada ya kuhudhuria kesi yake ya masuala ya ardhi kwao Burundi.

Tambwe alilazimika kusafiri hadi Burundi baada ya kuwa kuna mgogoro wa ardhi uliosababisha kufikia uamuzi wa kumalizana mahakamani.

"Ijumaa alikwenda kwenye kesi baada ya hapo atarejea Dar es Salaam kwa ajili ya kazi," alisema ndugu yake.

"Nafikiri mambo yataenda vizuri kwa kuwa wale jamaa waliingia katika kiwanja cha Tambwe na sasa mambo yanaenda vizuri."

Tupe Maoni Yako