Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Liverpool Yafuata Nyayo Za Tottenham Ni Kuhusu Uwanja


Klabu ya Liverpool imeamua kupanua uwanja wake wa Anfield inaoutumia sasa ili kuufanya kuhudumia mashabiki 60,000 tofauti na idadi ya sasa.
Awali uwanja huo ulitengenezwa ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 54,074 na ambapo mwaka 2016 upanuzi uliofanyika ulisaidia kuongeza idadi ya mashabiki 10,000.
Hivyo, Mkurugenzi wa Liverpool, Peter Moore alisema iwapo watapewa kibali wanatarajia kuongeza viti 6,000 zaidi ili kufanya idadi ya mashabiki kufikia 60,000.
Nayo klabu ya Tottenham kwa sasa bado inatumia mechi zake za nyumbani kwenye uwanja wa Wembley kutokana na kuendelea na ukarabati wa uwanja wake.

Tupe Maoni Yako