Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Dau La Usajili Wanalotaka Lipuli Kumwachia Kwasi Hili Hapa

Dau la Usajili wanalotaka Lipuli kumwachia Kwasi Hili hapa
Leo ni siku moja kabla ya dirisha dogo kufungwa rasmi mara baada ya tarehe ya mwanzo kuingia Mushkeli, Dirisha litafungwa rasmi kesho December 23, Saa tano na dakika 59.
Wakati huo Lipuli ikiwa imewaita Simba Mjini Iringa ili kujadili suala la usajili wa Asante Kwasi ambaye inadaiwa anamkataba bado na Lipuli licha ya Simba kusemekana kuwa nao washamsajili dau lake limeanza Kutajwa.
Inasemekana msomaji wa Kwataunit dau ambalo Lipuli wanataka ili kumwachia Asante Kwasi ni Kuanzia Milioni 50 za Kitanzania, Yani unaanza Milioni moja mpaka hamsini.
Taarifa hizi zimetoka kwa moja wa viongozi wa juu wa Klabu hiyo huku akisema mazungumzo ya bei pia yataruhusiwa ila dau lao litaanzia kwenye milioni 50.

Tupe Maoni Yako