Monday, December 4, 2017

Mawingu Tz

OZIL Mguu Pande Mguu Sawa Manchester United...Arsenal Kilio Tu


Rio Ferdinand amemkaribisha Mesut Ozil kujiunga na Manchester United katika dirisha dogo la usajili Januari, mwakani.
Ferdinand aliyekuwa nahodha wa Man United, amesema Ozil ana sifa za kucheza Old Trafford kwa kuwa ni mchezaji bora wa nafasi ya kiungo.
“Tunamkaribisha kwa moyo mmoja kwasababu ni mchezaji mwenye uwezo mzuri uwanjani, binafsi niliwahi kucheza naye akiwa Real Madrid ni mchezaji makini na hodari,” alisema Ferdinand.
Kauli ya nguli huyo wa zamani wa England imekuwa muda mfupi baada ya kocha wa Man United, Jose Mourinho kudai milango iko wazi kwa Mjerumani huyo.
Mchezaji huyo alijiunga na Arsenal mwaka 2013 kutoka Real Madrid akivunja rekodi kwa kutua Makao Makuu Emirates kwa Pauni 45 milioni. Mkataba wa Ozil unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Tupe Maoni Yako