Wednesday, December 6, 2017

Mawingu Tz

Tetesi Zote Za Usajili Kutoka Man United, Arsenal, Chelsea, Liverpool, Barca, Madrid n.k

Eden Hazard
Mazungumzo baina ya Chelsea na Eden Hazard kwa ajili ya mkataba mpya yamesimama kwani Mbelgiji huyo anataka kutimkia Real Madrid kwa mujibu wa The Times .
Imeripotiwa kuwa Blues wapo tayari kumfanya Hazard kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, kwa mshahara wa £300,000 kwa wiki.
Lakini Hazard anasita kuongeza mkataba na bado amebakiwa na miaka miwili na nusu kwani anahofu kukosa kutimiza ndoto ya kujiunga na Los Blancos.

MADRID WANAFIKIRIA KUMTOA KROOS WAMPATE DYBALA


Paulo Dybala Juventus
Rais wa Real Madrid Florentino Perez anafikiria kumtoa Toni Kroos kwa Juventus ili ampate Paulo Dybala kama biashara ya kubadilishana, kwa mujibu wa  Rai Sport .

COURTOIS KUONDOKA BURE CHELSEA


Thibaut Courtois
Thibaut Courtois ataruhusiwa kuondoka kama mchezaji huru Chelsea ifikapo 2019 kwani Mbelgiji huyo ameendeea kukataa kusaini mkataba mpya kwa mujibu wa, The Sun .
Ikiwa Blues watashindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mlinda mlango huyo – ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Real Madrid – atalazimika kumaliza mkataba wake badala ya kumuuza kabla ya kuumaliza mkataba.

MAN UTD WANAMTAKA BALE KWA NUSU BEI


Gareth Bale Real Madrid
Manchester United wataachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale kama Real Madrid hawataipunguza hadi nusu bei ya Gareth Bale, kwa mujibu wa  The Mirror .
Los Blancos wanaamini thamani ya Bale ni £100 milioni, lakini Mashetani Wekundu wanataka saini yake kwa £50-60m.

JUVENTUS YAMTAKA KINDA WA KIBRAZILI


Eder Militao Brazil 2015
Imeripotiwa kuwa Juventus wanamfuatilia kinda wa Kibrazili anayekipiga Sao Paulo, Eder Militao wakiwa na lengo la kumleta Turin, kimedai  calciomercato.com .
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akicheza mechi nyingi kwenye klabu ya Dorival Junior, kama beki mpya. Militao pia anaweza kucheza kama beki wa kati na kiungo.

PALACE WANAMTAKA KIPA WA PSG


Kevin Trapp Paris Saint Germain
Crystal Palace ambao wapo kwenye hatari ya kushuka daraja Ligi Kuu Uingereza wamegeuzia macho yao kwa mlinda mlango wa Paris-Saint Germain Kevin Trapp, kwa mujibu wa Sun .

 STERLING KULAMBA PAUNDI 300,000


Raheem Sterling Manchester City
Manchester City wanajipanga kumfanya Raheem Sterling kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye Ligi ya Uingereza kwa kumlipa £300,000 kwa wiki, kwa mujibu wa  The Sun .

CHELSEA WANAMTAKA AUBAMEYANG


Pierre-Emerick Aubameyang Borussia Dortmund.jpg
Meneja wa Chelsea Antonio Conte yupo tayari kupigana vikumbo na Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, kwa mujibu wa  Sunday Express

NEYMAR AMEPEWA DILI REAL


Neymar PSG Troyes Ligue 1 29112017
Neymar amefikia makubaliano na rais wa Real madrid Florentino Perez ambayo yatamwezesha kujiunga na miamba hiyo ya Hispania 2019, kwa mujibu wa  Don Balon .

SANDRO AIFUNGULIA MILANGO CHELSEA


Alex Sandro Juventus
Alex Sandro ameendelea kuwaachia mlango wazi Chelsea kwani anafikiria kuondoka Juventus baada ya Kombe la Dunia 2018, kimedai TMW .
Beki huyo mahiri amekuwa akihusishwa sana na tetesi za kujiunga na Blues dirisha la majira ya joto na kiwango chake Kombe la Dunia akiwa na Brazili ndicho kitakachoweza kumsaidia kutua London.

MOURINHO ANAMTAKA OZIL OLD TRAFFORD


Mesut Ozil Arsenal
Bosi wa Manchester United Jose Mourinho anamtaka Mesut Ozil kwenye kikosi chake ili kutatua matatizo ya nafasi ya namba 10, kwa mujibu wa Telegraph .
Nyota huyo wa Arsenal atakuwa amemaliza mkataba wake majira ya joto na anasita kusaini mkataba mwingine, jambo linalowafanya wengi wahofu kwamba ataondoka.

COUTINHO KULIPWA €14M KWA MWAKA BARCA


Philippe Coutinho Liverpool
Barcelona watampa Philippe Coutinho mkataba wenye thamani ya €14 milioni kwa msimu ikiwa watafanikiwa kuishawishi Liverpool kumuuza Mbrazili huyo, kimedai  Sport .
Liverpool walikataa ofa zote kwa ajili ya Coutinho majira ya joto, lakini Barca wanataka kurudi upya Januari na wapo tayari kutoa ofa ya €150m kwa ajili ya kiungo huyo.
Lakini kusajiliwa kwa Coutinho kuuza wachezaji watatu ili kuweza kumudu bajeti yao.

MADRID KUMSAJILI VINICIUS 2018


Vinicius Junior
Real Madrid watakamilisha usajili wa kinda wa Kibrazili Vinicius Junior msimu ujao wa majira ya joto, kwa mujibu wa AS .
Madrid walikubali dili la €45 milioni kwa ajili ya Vinicius wa Flamengo mwezi Mei, lakini mshambuliaji huyo hawezi kuruhusiwa kuhama hadi atakapotimiza umri wa miaka 18 Julai mwakani.

ARSENAL NA MAN CITY ZAMWANIA EVANS


Jonny Evans West Brom
Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans amezivutia Manchester City na Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa  The Telegraph .
Ilitipotiwa kuwa ofa ya Arsenal ya £25 milioni ilikataliwa Agosti 31 kwa ajili ya mchezaji huyo, kwani WBA wanataka kiasi kisichopungua £30m.

MAN UTD YAMTOLEA MACHO CRISTANTE


Bryan Cristante Italy
Manchester United inataka kumsajili kiungo wa Atalanta, Bryan Cristante kuwa mrithi wa Marouane Fellaini, kwa mujibu wa  The Sun .
Mashetani Wekundu wapo tayari kumpoteza Fellaini na kiwango cha Cristante akicheza kwa mkopo Serie A kimemshawishi Mourinnho kuamini kuwa mchezaji huyo ni mbadala sahihi kwa Fellaini.
Atalanta wana uwezo wa kumsajili Cristante kutoka klabu yake mama Benfica kwa paundi milioni 10 mwisho wa msimu, na kisha kumuuza kiungo huyo Man United kwa paundi milioni 31.

MADRID WATAJA TAREHE YA MWISHO KUMSAJILI DE GEA


David De Gea Manchester United 2017
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameweka tarehe ya mwisho majira ya joto 2018 kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea, kwa mujibu wa  Diario Gol .

COUTINHO KWA AJILI YA BARCELONA PEKEE?


Philippe Coutinho Liverpool 2017
Wakuu wa Barcelona wameungana kuhakikisha Philippe Coutinho anasaini mkataba kujiunga na klabu hiyo Januari, kwa mujibu wa Sport .
Mesut Ozil amependekezwa kuwa mbadala Barce ikiwa miamba hao wa Catalan watashindwa kuishawishi Liverpool kumuuza Coutinho dirisha dogo la uhamisho.
Lakini habari zimedai kuwa Coutinho bado anataka kuondoka Anfield, na kwamba ofa itakayofikia €150 milioni itatosha kuishawishi Liverpool kumuuza, na Liverpool haitaki kufikiria mchezaji mwingine tofauti.

ARSENAL KUMSAJILI FEKIR


Nabil Fekir Lyon
Arsenal itafanya mpango wa kumsajili Nabil Fekir kutoka Lyon, kwa mujibu waTuttoMercatoWeb .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa amekuwa akifuatiliwa na Barcelona, Juventus na Atletico Madrid, lakini Gunners wanatumai kumsajili kuwa mshambuliaji wao.

ARSENAL WANAPEWA NAFASI KUBWA KUMSAJILI JANKTO


Jankto Udinese Chievo
Arsenal wanapewa nafasi kubwa kumsajili Jakub Jankto kutoka Udinese baada ya Juventus kuacha mpango wa kumsajili, kwa mujibu wa  Calciomercato .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akifuatiliwa na klabu zote mbili, lakini miamba wa Serie A hawapo kutoa fedha nyingi kumsajili hivyo kuwaachia Gunners nafasi.

FONSECA AITOSA EVERTON


Paulo Fonseca, Shakhtar Donetsk
Paulo Fonseca ameikataa fursa ya kuwa meneja mpya wa Everton, kwa mujibu wa  Football Insider .
Meneja huyo wa zamani wa Porto ameibukia kuwa na nafasi kubwa kuirithi nafasi ya Ronald Koeman katika Goodison Park, lakini amekataa ofa ya kuwanoa Toffees ili kuendelea na Shakhtar Donetsk.

SANE KULAMBA DILI MPYA CITY


Leroy Sane Manchester City
Manchester City watampa Leroy Sane mkataba mpya ambao utamwezesha kulipwa £80,000 kwa wiki, kwa mujibu wa  The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Pep Guardiola tangu ajiunge na City akitokea Schalke na mshahara kwae utapandishwa sasa, lakini atalazimika kuwasubiri Kevin De Bruyne, David Silva na Fernandinho kusaini mataba mpya kwanza.

MADRID YAJIPANGA KUMSAJILI LUIZ


David Luiz Chelsea
Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa Chelsea dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Daily Telegraph .
Luiz amekosa maelewano mazuri na meneja wa Blues Antonio Conte katika wiki za hivi karibuni, jambo linaloashiria anaweza kuwekwa sokoni majira ya baridi.
Madrid nao wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya mwanzo mbaya msimu huu.

DORTMUND WANAMTAKA KINDA WA UNITED


Angel Gomes England
Borussia Dortmund wameonyesha nia ya kumsajili kinda wa Manchester United Angel Gomes, kwa mujibu wa The Sun .
Gomes bado hajasaini mkataba mpya na United na anaweza kuondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu, Barcelona ni miongoni mwa klabu zinazoitamani huduma yake.
Dortmund sasa wanafikiria kumsajili Gomes baada ya kumsajili kinda mwenzake wa Uingereza Jadon Sancho kutoka Manchester City.

BARCA WANAMTAKA ERIKSEN


Christian Eriksen Tottenham Bournemouth EPL 14102017
Barcelona wapo tayari kutoa dau nono uhamisho wa Januari kumsajili kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, kwa mujibu wa Don Balon .
Ingawa wamehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Mesut Ozil na Philippe Coutinho, wanaamini kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark anaweza kuongeza nguvu zaidi kwenye kikosi chao na mbinu zaidi ya wapinzani wao.

PEP KUIMARISHA SAFU YA ULINZI


Sergi Roberto Inigo Martinez Real Sociedad Barcelona 201617
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amegeuza macho yake kwa beki wa Real Sociedad Inigo Martinez akijipanga kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa Januari, kwa mujibu wa  The Sun .

SPURS WANAMTAKA MASINA KUWA MBADALA WA ROSE


Adam Masina Bologna
Adam Masina anaweza kuhama kutoka Bologna kwenda Tottenham uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Spurs wanaamini beki huyo anaweza kuwa mbadala sahihi kwa Danny Rose, ambaye anaendelea kuhusishwa na tetesi za kutimkia Manchester United.
Mauricio Pochettino pia anataka kumsajili mshambuliaji kinda na macho yake yamedondoka kwa Breel Embolo wa Schalke.

PSG YAIPIKU MAN CITY MBIO ZA ALEXIS


Alexis Sanchez Arsenal
Paris Saint-Germain inaitangulia Manchester City katika mbio za kumfukuzia nyota wa Arsenal Alexis Sanchez Januari, The Mirror limeripoti.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile unafikia ukomo mwisho wa msimu huu, na PSG imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajli kwa mkataba wa awali wanapojipanga kumruhusu Neymar kwenda Real Madrid msimu ujao wa majira ya joto.

SHAW MBIONI KUONDOKA UNITED KWA MKOPO


Luke Shaw Manchester United 200917
Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw anajipanga kujiunga na Newcastle kwa mkopo kwa mujibu wa habari kutoka  the Daily Mirror .

REAL MADRID KUTOA DAU LA £80M KUMSAJILI MARTIAL


Martial celebration
Real Madrid wapo tayari kutoa kitita cha £80 milioni kwa ajili ya kumsajli Anthony Martial msimu ujao majira ya joto, kwa mujibu wa

Tupe Maoni Yako