Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Elias Maguli amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Polokwane City inayoshiriki liki kuu ya Afrika Kusini (PSL) akiwa kama mchezaji huru.
Kabla ya kuijiunga na Polokwane, Maguli aliwa akiitumikia Dhofar FC ya Oman tangu mwezi June 2016 akitokea Stand United ya mkoni Shinyanga.
Kukamilika kwa dili hilo la kujiunga na Polokwane kunamaliza tetesi za striker huyo kujiunga na vilabu vya Simba na Yanga ambavyo awali vilihusishwa kuwania saini yake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili nchini.
Maguli anaungana na Abdi Banda anaekipiga Baroka FC ya Afrika Kusini huku wote kwa pamoja wakiwa ni wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. kwa sasa Maguli yupo na timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ inayoshiriki michuano ya kombe la Chalenji nchini Kenya.
Polokwane baada ya kucheza mechi 11 kwenye ligi ya Afrika Kusini imefanikiwa kuvuna pointi 11 ikiwa imeshinda michezo miwili pekee, sare tano na imeshapoteza mechi nne, inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi. Katika mechi hizo 11, mefunga magoli 12 na kuruhusu magoli 15 hivyo kufanya wastani wa magoli kuwa hasi tatu (-3).
Akiwa Tanzania, Maguli amewahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting, Simba na Stand United vyote vikiwa vinashiriki ligi kuu (VPL).
Tupe Maoni Yako