Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Simba Yafunguka Mazito Suala La Mavugo Kutemwa

Kamati ya Usajili ya Simba, imetangaza kumbakiza kundini mshambuliaji wake Laudit Mavugo raia wa Burundi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema baada ya kumtema beki Method Mwanjale, hawana mpango wa kumuacha mchezaji mwingine.

Hans Poppe amesema Simba haina mpango wa kumuacha mchezaji licha ya kuelezwa kwamba Mavugo analazimika kumpisha Dayo Domingues kutoka Msumbiji.


“Hatuna mpango wa kumuacha mtu yoyote baada ya Mwanjali, hivyo baada ya usajili wa Kwasi kukamilika, hatutakuwa na usajili mwingine,” alisema.

Tupe Maoni Yako