Saturday, December 2, 2017

Mawingu Tz

RASMI:Huyu Hapa Mkomola Ndani Ya Uzi Wa Jangwani..Umesikia Alichosema Hussein Nyika Baada ya Usajili Huo?

Yanga tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wawili katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Wakwanza alikuwa mlinzi mahiri wa kati Fiston Kayembe Kanku kutoka DRC ambaye amejaza nafasi moja ya Kimataifa iliyokuwa imebaki.
Wapili ni mshambuliaji kinda Yohana Nkomolla aliyesajiliwa kutoka kikosi cha timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes iliyoshiriki michuano ya AFCON U17 mapema mwaka huu nchini Gabon.
Nkomolla ametambulishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika na kumkaribisha rasmi katika familia ya Yanga.
Nyika amelitaka benchi la ufundi kuhakikisha linalinda kipaji cha mshambuliaji huyo kinda kwani ni hazina kubwa ya Yanga baadae.
“Tunahitaji kuwa na vijana ambao watakuwa wakiwa ndani ya klabu,hii itawafanya kujua misingi na utamaduni wetu Kabla kuwa wachezaji wakubwa baadae, ana kipaji kikubwa,ni jukumu la benchi la ufundi kukiendeleza kwa manufaa ya klabu siku za usoni,” alisema Nyika.
Uongozi wa Yanga umedhamiria kukisuka upya kikosi chake ambapo sasa kimesheheni idadi kubwa ya wachezaji vijana ambao watakuwa tegemeo siku za usoni.
Baadhi ya wachezaji vijana walio chini ya umri wa miaka 23 ndani ya kikosi cha Yanga sasa ni pamoja na Benno Kakolanya, Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Maka Edward, Geofrey Mwashiuya, Emanuel Martin, Said Mussa, Baruani Yahya, Juma mahadhi, Matheo Antony, Said Juma, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Raphael Daudi, Obrey Chirwa, Yohana Nkomolla, Ibrahim Ajib na Yusuph Mhilu


Tupe Maoni Yako