Ukisema amesawazisha si vibaya maana Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo yake ya tano ya Ballon d’Or.
Ushindi huo unamfanya kufikisha tuzo tano sawa na Lionel Messi.
Shughuli ya utoaji tuzo imefanyika katika mnara maarufu wa Eiffel jijini Paris, Ufaransa.
Ronaldo nyota wa Real Madrid na nahodha wa Ureno, alionekana ni mwenye furaha, alipanda jukwaani na baadaye kufuatiwa na mama yake mzazi na mwanaye wa kwanza.
Tupe Maoni Yako