Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Kumbe Wachezaji Man United, Man City Walizichapa, Kocha Akapasuliwa, Mourinho Akapigwa Chupa

Kocha wa Man United, Jose Mourinho alivamia katika chumba cha Man City baada ya kupigwa chupa akimtuhumu mmoja wa wachezaji wa City.

Imebainika wachezaji wa Manchester United na wale wa Manchester City walizichapa ile mbaya baada ya mechi yao Jumapili.

Katika mechi hiyo, licha ya kutangulia kufunga, Man United walilala kwa mabao 2-1.

Baada ya mechi, wakati wakirejea vyumbani, wachezaji hao walitwangana na inaelezwa kocha msaidizi wa Man City, Mike Arteta alipasuliwa katika paji la uso.

Tupe Maoni Yako