Friday, December 1, 2017

Mawingu Tz

Javier Mascherano Amtaja Mchawi Alisababisha Kuondoka Liverpool

Mwaka 2010 kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool Javier Mascherano aliingia katika mzozo mkubwa na klabu ya Liverpool baada ya kudaiwa kwamba alikuwa akilazimisha kuachana na klabu hiyo.
Baadaye Mascherano alijiunga na Barcelona, miaka saba sasa imepita tangu tukio hilo litokee na Mascherano hakuwahi kulizungumzia lakini sasa amefunguka nini haswa kilitokeoa katika kipindi hicho.
Mascherano amedai kwamba Rafael Benitez alikuwa sababu ya yeye kuondoka Liverpool, Mascherano anaamini kwamba Benitez alikuwa akimuamini sana na baada ya kocha huyo kuondoka alikosa raha na kutamani kumfuata.
Mascherano anasema baada ya Benitez kujiunga na Inter Millan na yeye akawa na lengo la kwenda Italia kukipiga Inter Millan na mazungumzo yalishaanza lakini yalionekana kusua sua sana.
“Baadae Barcelona walikuja, niliamua kupambana ili kujiunga nao. Klabu kama hii huwa ni ngumu kukutafuta mara mbili mfululizo, wakikukosa mara moja huwa wanatafuta mwingine na niliogopa hilo kutokea” alisema Mascherano.
Mascherano hana msimu mzuri Barcelona msimu huu akiwa amefanikiwa kuanza katika michezo saba tu na sasa anaamini muda wake wa kuwa Barca pengine unaelekea ukingoni lakini anatamani kama akiondoka Barca aondoke kwa wema.

Tupe Maoni Yako