Sunday, December 3, 2017

Mawingu Tz

VIDEO:Haji Manara Akizungumzia Mchakato Wa Usajili Simba (Dirisha Dogo).

Mkuu wa idara yahabari na mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara amesema Simba ni lazima ifanye usajili katika kipindi hiki.
Manara amesema tayari ripoti ya benchi la ufundi imeshafika kwa kamati ya usajili ambako wanamalizia mchakato wa nani asajiliwe kisha wapeleke kwenye kamati ya utendaji.
“Simba itaongeza mchezaji, tumeshapokea ripoti ya benchi la ufundi ipo kwenye kamati ya usajili na wao wapo kwenye kumalizia mchakato. Nadhani wiki ijayo kamati ya utendaji itaridhia bila shaka na tutatangaza nani anaingia.”
“Nani ataingia mimi sijui, lakini tutasajili bila shaka lazima tutaongeza mchezaji. Yanayoandikwa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii ni tetesi. Tetesi kwenye kipindi cha usajili ni jambo la kawaida dunia nzima, mimi sina tatizo nalo.”
Matokeo Mechi Zote EPL leo Jumamosi Decemba 2 2017..Mourinho Mwamba Mbele Ya Wenger
BOFYA HAPA KUMTAZAMA MANARA AKIZUNGUMZIA MFUMO MPYA…


Tupe Maoni Yako