Friday, December 15, 2017

Mawingu Tz

Familia Yamuondoa George Lwandamina Yanga, Kuondoka Alfajiri

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, anatarajia kuondoka nchini Tanzania alfajiri ya kesho Ijumaa kuelekea nchini Zambia.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema Lwandamina anaelekea kwao kwa ajili ya masuala ya kifamilia.
Lwandamina ambaye ni raia wa Zambia aliyetua Yanga akichukua nafasi ya Hans Van Pluijm ambaye kwa sasa yupo Singida United alikuwa katika mapumziko ya siku kadhaa kutokana na kuwapa nafasi wachezaji wake wapumzike kufanya mazoezi tangu juzi.
Akifafanua zaidi, Mkwasa alisema: “Kocha anaondoka nchini kesho alfajili anaenda kwao Zambia kwa ajili ya mambo ya kifamilia kama nilivyosema, na baada ya hapo anarejea na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.”
Mkwasa ameongeza kuwa baada kuwa kocha huyo baada ya kumaliza mahafari ya bintiye atarejea Jumatatu huku timu ikiwa chini ya Kocha Msaidizi Shadrack Nsajigwa.


Tupe Maoni Yako