Thursday, November 16, 2017

Mawingu Tz

Tetesi za Usajili Simba:Hawa Lazima Watue Simba Dirisha Dogo..Yahusishwa Na Straika Hatarii


KLABU ya Simba inatajwa kuwa katika RADA za mwisho mwisho kushusha vifaa viwili vya kimataifa kutoka nchini Rwanda ili kujiimarisha zaidi katika safu yao ya Ushambuliaji na kujihakikishia suala la ukame wa mabao linaisha kabisa katika kikosi cha Simba.

Kwa taarifa toka ndani ya klabu ya Simba ambazo kwataunit.com tumezipata wachezaji wanaoweza kusajiliwa Simba au mmoja wapo kusajiliwa ni Shasir Nahimana ambaye ni nyota wa klabu ya Rayon Sports akisifika kufunga.

Mwingine ambaye anatarajiwa huenda akasajiliwa na Simba ni Kelvin Muhire ambaye anacheza namba nyingi awapo uwanjani lakini ni mzuri zaidi akicheza kama namba 10. 
Image result for muhire kelvin
Hapa  Muhire Kelvin akiwania Mpira na Shiza Kichuya timu ya Taifa

Taarifa zaidi zinasema wachezaji hao ni mchongo wa kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma ambaye anawajua vyema kutokana na kuwa wamewahi kupita katika mikono yake akiwa kama kocha wao.

Simba inahaha kupata wachezaji wazuri wa kufunga magoli ili Bocco na Okwi kupata wasaidizi sahihi kwani Mavugo,Luizio na Mghana Gyan wameshindwa kutoa matokeo chanya waliyotarajia katika kikosi chao.

Wachezaji hao wanapewa nafasi kubwa kwani inaaminika chaguo la kocha huwa ni chaguo linalosikilizwa zaidi na viongozi ambao kazi yao kubwa huwa inakuwa ni utekelezaji tu.

Tupe Maoni Yako