Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Yanga Itawakosa Nyota Hawa Wanne Jumapili Kwenye Kombe La Shirikisho AZAM

Klabu Bingwa Nchini Yanga itawakosa Nyota wake wanne ambao ni majeruhi Jumapili Hii itakapocheza kombe La Shirikisho dhidi ya Reha Fc.
Wachezaji hao watakaokosekana ni Thaban Kamusoko ambaye ni majeruhi kwa takribai miezi miwili sasa , Kelvin Yondani ambaye aliumia timu ya Taifa,
Mwingine ambaye ataukosa mchezo huo ni Mzimbabwe Donald Ngoma ambaye anaukosa mcheo huo sababu za kuwa majeruhi.
Na mchezaji mwingine ambaye ataukosa mchezo huo ni Pato Ngonyani ambaye ni majeruhi Pia.
Hata Hivyo daktari wa timu ya Yanga Edward Bavu amesema kuwa hiyo ni ripoti ya mpaka muda Huu lakini kutokana na baadhi ya wachezaji katika list hiyo kuwa tayari wameshaanza mazoezi mepesi kuna uwezekano baadhi yao wakaingia kwenye Kikosi.
Yanga itacheza na Reha Fc inayoshiriki ligi daraja la Pili katika michuano ya Azam HD Federation Cup, michunao ambayo Bingwa mtetezi ni Simba.

Tupe Maoni Yako