Thursday, December 21, 2017

Mawingu Tz

MAJANGA:Kamusoko Apishana Na Ibrahim Ajibu Yanga

Wakati washabiki wa Yanga wakiwa na furaha baada ya kumuona kiungo wao Thaban Kamusoko akirejea katika mazoezi ya timu hiyo siku ya jana, Kiungo huyo amepishana na mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib ambaye yeye jana hakutokea kutokana na Kuumwa Malaria.
Kamusoko alikaa nje ya kikosi cha mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Bara Yanga takribani miezi miwili kabla ya jana kuanza mazoezi mepesi ambayo yametia moyo benchi la ufundi.
Yanga toka kuanza kwa msimu imekabiliwa na majeruhi wengi hali iliyofanya kocha George Lwandamina kukosa kikosi chake cha kwanza cha moja kwa moja.
Yanga leo msomaji wa Kwataunit.com wanatarajia kuendelea na mazoezi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.

Tupe Maoni Yako