Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Mourinho Aionyesha Jeuri Real Madrid Vita Ya Hazard

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameamua kumfungia kazi mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard kwa kutaka kumrudisha kwenye himaya yake.
Mourinho ameingia kwenye vita hiyo ya kutaka kumsajili nyota huyo, huku akijua kwamba tayari Chelsea imempandia dau baada ya kumuahidi kumpa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka minne.
Ofa hiyo mpya ya Hazard itategemea na uamuzi wake kuendelea kubaki Stamford Bridge.
Hata hivyo, Mourinho amejikuta akipambana na timu vigogo za Real Madrid, PSG ambazo zimeshatua kumuwinda nyota huyo.

Tupe Maoni Yako