Thursday, December 7, 2017

Mawingu Tz

Huyu Ndo Kinda anaezitesa Simba, Yanga msimu huu


UMUHIMU wa kuwepo kwa matangazo ya moja kwa moja ya soka ni mkubwa kwa hata wachezaji wa Ligi Kuu Bara na hiyo kumbe ndiyo siri ya Eliuter Mpepo wa Tanzania Prisons kuzitesa Simba na Yanga.
Mpepo ambaye staili yake ya uchezaji inahusisha nguvu nyingi amejipatia umaarufu baada ya kuisumbua ngome ya ulinzi ya Simba kabla ya kuja kuifunga Yanga kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Huu ni msimu wa kwanza kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kucheza Ligi Kuu akitokea Mbeya Kwanza ambayo inashiriki daraja la kwanza, mpaka sasa Mpepo ameifungia timu yake mabao 3 ndani ya michezo 7.
Hata hivyo mshambuliaji huyo alimtaja Athuman Mchupa kama mshambuliaji wake ambaye alikuwa akimhusudu na kujifunza mengi wakati akianza safari yake ya kucheza soka.


Tupe Maoni Yako