Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Hatimae Ngoma Arejea Nchini..Yanga Wanajipanga Kutoa Tamko Kali Dhidi Yake

Baada ya sintofahamu ya wiki kadhaa hatimaye mshambuliaji ‘mtukutu’ wa Yanga Donald Ngoma amarejea jijini Dar es salaam.
Ngoma amereja Dar jana akitokea kwao Zimbabwe akidaiwa kuondoka ‘kimyakimya’ bila kuutaarifu uongozi wa Yanga.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alieleza kusikitishwa na tukio hilo na kusisitiza mshambuliaji huyo atakumbana na adhabu kubwa kama utetezi wake hautauridhisha uongozi.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema uongozi utatoa taarifa ya nini kimeafikiwa juu ya hatma ya mshambuliaji huyo.

Tupe Maoni Yako