Thursday, December 7, 2017

Mawingu Tz

Hizi Ndo Takwimu Za Msuva Morocco….Anawakimbiza Balaa

JAMAA ndio basi tena ameshalisoma na kulielewa soka la Morocco. Takwimu za winga wa DH El Jadidi, Simon Msuva kwenye ligi kuu nchini humo tangu ajiunge nao zinatosha kusema ameiweza ligi hiyo.
Msuva alisajiliwa na waarabu hao Agosti mwaka huu akitokea kwa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga lakini kwa kipindi kifupi tu ameonesha yeye si mtu wa kusubiri kuzoea mazingira.
Msaada kwa timu

Mara kadhaa Msuva amekuwa aidha akifunga au kutoa pasi ya bao linaloamua mchezo. Jambo hili limemfanya winga huyo mwenye kipaji kingine cha kucheza muziki hasa wa Bongo Flava, awe na heshima yake katika klabu hiyo.


Jino kwa jino na mastraika

Licha ya muda mwingi kuchezeshwa kama winga na mara chache kama mshambuliaji namba mbili, Msuva ameendelea kuwabana mbavu mastraika katika ligi hiyo kwa idadi ya mabao.

Naghmi Mehdi anaongoza orodha ya wafunganji katika ligi hiyo akiwa na mabao sita huku Hamid Ahedad anayefuatia kwa mabao (5) akiwa amemzidi Msuva kwa bao moja tu hali inayoonesha winga huyo ‘akikaza’ ana uwezo wa kuibuka mfungaji bora.
Mashine ya kutengeneza mabao

Licha ya kutupia mabao manne katika mechi tisa alizoshuka dimbani na timu hiyo, Msuva tayari amesaidia upatikanaji wa mabao mengine matatu kwenye ligi kuu nchini humo maarufu kama Botola.


Kikosi bora cha ligi kuu nchini Morocco Novemba, 2017
Atinga kikosi bora cha mwezi

Usidhani anaheshimika El Jadidi tu, familia nzima ya wapenda soka nchini Morocco wanaijua shughuli yake aliyoifanya tangu atue nchini humo.

Kwa mara ya kwanza Msuva amefanikiwa kuingia katika kikosi bora cha ligi akitajwa kama winga wa kulia kwenye kikosi cha mwezi Novemba.
Msuva alianza kung’ara kwenye kikosi cha pili cha Azam FC kabla hajatimkia Moro United ya mjini Morogoro ambako Yanga walimuona na kumpa mkataba

Tupe Maoni Yako