Thursday, December 7, 2017

Mawingu Tz

Yanga Na Simba Wapata Vibonde Kombe La Azam Sports Federation..Ratiba Kamili Hii Hapa

Gwiji wa soka nchini, Kenneth Pius Mkapa (kushoto) akionyesha karatasi inayomtambulisha mpinzani wa Yanga, Reha FC. Kulia ni gwiji mwingine, Bitta John aliyeichagua YangaMABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Green Worriers, zote za Dar es Salaam katika mchezo wa Raundi ya Pili ya Kombe la Azam Sports Federation kati ya Desemba 20 na 25 mwaka huu Jijini.


Mahasimu wao, Yanga watamenyana na Reha FC katika hatua hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 64, wakati Azam FC watamenyana na Area C ya Dodoma Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Katika droo iliyopangwa leo studio za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam, ikiongozwa na wachezaji nyota wa zamani nchini, makipa Steven Nemes, Mwameja Mohammed, beki Kenneth Mkapa na mshambuliaji Bitta John, washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC watamenyana na Makanayagio FC ya Rukwa.
Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Madini FC, Abajalo wataikaribisha Tanzania Prisons, Njombe Mji wataikaribisha Mji Mkuu, Boda Boda FC ya Arusha watakuwa wenyeji wa Singida United na Mwadui FC wataikaribisha Pepsi FC.


RATIBA KAMILI RAUNDI YA PILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP
Ruvu Shooting Vs Madini FC 
Abajalo Vs Tanzania Prisons
Njombe Mji Vs Mji Mkuu
Singida United Vs BodaBoda
Mwadui FC Vs Pepsi
Maji Maji FC Vs New Generation
Boma FC Vs Ndanda FC
Stand United Vs AFC Arusha
Burkina Faso FC Vs Lipuli FC
Green Worriers Vs Simba SC
Azam FC Vs Area C
Yanga SC Vs Reha FC
Mbeya City Vs Ihefu
Villa Squad Vs Mtibwa Sugar
Kagera Sugar Vs Makambako
Makanayagio Vs Mbao FC 
JKT Mlale Vs KMC
Ambassador Vs JKT Oljoro
Mshikamano Vs Polisi Tanzania
Rhino Vs Alliance 
Ashanti United Vs Friends Rangers
Toto Africans Vs Eleven Stars
Maji Maji Rangers Vs Mbeya Kwanza
Milambo FC Vs Buseresere FC
African Lyon Vs Kiluvya United
Biashara United Vs Mawenzi Market
Mvuvumwa Vs JKT Ruvu
Coastal Union Vs Dodoma FC
Polisi Dar Vs Mgambo JKT
Kariakoo United Vs Transit Camp
Shupavu Vs Real Moja Moja
Mufindi FC Vs Pamba SC 


Tupe Maoni Yako