Thursday, November 16, 2017

Mawingu Tz

Haruna Niyonzima Atoa Ya Moyoni Baada Ya Chirwa Kupewa Tuzo Ya Uchezaji Bora Mwezi Octoba

BAADA ya straika wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba katika Ligi Kuu Bara, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, amesema tuzo hiyo imefika sehemu iliyostahili.


Chirwa ambaye aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, katika kuwania tuzo hiyo, amewashinda Erasto Nyoni wa Simba na Ibrahim Ajibu wa Yanga.

 Niyonzima alisema hafahamu vinatumika vigezo gani kumpata mshindi wa tuzo hizo, lakini Chirwa anafaa kuwa mshindi kwa mwezi huo kwani hata katika mechi dhidi yao alionyesha kiwango kizuri.

“Chirwa kupewa uchezaji bora wa mwezi hajapendelewa bali amestahili kwani nimemuona katika mchezo waliocheza dhidi ya Stand United kule Shinyanga alipambana sana pamoja na kufunga bao moja.

“Utaona hadi siku hiyo Yanga inaibuka kwa ushindi wa mabao manne mchango wake ulikuwa mkubwa sana pia hata kwenye ‘derby’ yetu aliisaidia sana Yanga,” alisema Niyonzima.

Tupe Maoni Yako