Saturday, December 23, 2017

Mawingu Tz

Hapa Ndo Ilipofikia Safari Ndemla Kwenda Sweden...mmmh


Hivi karibuni kiungo wa Simba, Said Ndemla alifuzu majaribio yake katika klabu ya AFC Eskilstuna ya nchini Sweden, lakini dili la kumalizana kati ya Simba na timu hiyo limechukuwa muda mrefu na kuzuia maswali kwa baadhi ya wadau wa soka.
Mbali na hilo habari zinadai kuwa uongozi wa Simba ulighairi kumuuza mchezaji wao, lakini Meneja wake Jamal Kisongo amesema kuwa dili hilo bado lipo pale pale kwani Rais wa klabu hiyo atatua nchini muda wowote.
Katika uchunguzi ambao umefanywa na mwanaspoti ni kwamba Rais wa klabu hiyo ana mazungumzo pia na uongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) hii ya vijana wa timu ya Serengeti Boys ambao wanatakiwa kwenda kwenye vituo vya soka katika nchi tofauti ili kuwajenga zaidi kisoka na Sweden ni nchi mojawapo inayotajwa.
Hata hivyo haijajulikana kama Rais huyo atawasili lini nchini ila amewatuliza juu ya ishu ya Ndemla kuwa atakuja kuimaliza atakapofanya ziara yake hiyo kwani wana imani na Ndemla na hawana haraka naye kama watu wanavyodhani na kupelekea kukata tamaa.
Meneja wa Ndemla alisema kuwa anachokufahamu mpaka sasa kuwa uongozi wa AFC utakuwa nchini kumalizana na Simba labda itokee mabadiliko hapo baadaye.
"Watu wanapenda kuona mchezaji anapiga hatua mbele na ukizingatia alifuzu majaribio hayo, kilichopo sasa ni kuwasubiri viongozi wa timu ili waje wamalizane na Simba, sifahamu ni lini ila wametueleza kuwa tusubiri.
"Awali walishindwa kuja kutokana na matatizo yaliyokuwa yakiwakabili ikiwemo mmoja wao kupatwa na msiba, kukiwa na tofauti ama mabadiliko yoyote yatakayomfanya Ndemla ashindwe kwenda kucheza Sweeden yatawekwa wazi bila kificho maana mambo ya mpira hayajifichi," alisema Kisongo.

Tupe Maoni Yako