Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Simba Yawatupa Jukwaani Okwi, Niyonzima

KOCHA wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa kutokana na mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi raia wa Uganda kutokuwa sawa, amelazimika kumpatia mazoezi ya peke yake ili kumuweka fiti huku akitarajiwa kukosa mechi dhidi ya Ndanda mchezo ambao pia ataukosa Haruna Niyonzima.
Haruna Niyonzima.
Okwi alipatwa na majeraha ya enka hivi karibuni katika mechi dhidi ya Mbeya City ambapo bado anaendelea na matibabu. Akizungumza na Championi Jumatano, Masoud alisema kuwa, Okwi bado hayupo fiti hivyo amemua kumpatia programu maalumu ya kumweka fiti kutokana na majeraha yake ili aweze kurejea katika kiwango chake.

“Okwi bado hayupo fiti na hajaanza mazoezi pamoja na wenzie kwa sasa kuna mazoezi nimempatia ambayo anayafanya peke yake ya kuzunguka uwanja pamoja na viungo huku akiendelea kuwa karibu na dokta kwa lengo la kuangalia afya yake.

“Siwezi kumtumia mchezaji akiwa bado hajapona vyema kwani nitaweza kumuongezea majeraha zaidi na kuharibu uwezo wake, hivyo sitarajii kumtumia dhidi ya Ndanda hadi hapo atakapofanikiwa kuwa fiti. “Ukiachana na yeye pia kuna Niyonzima hayupo sawa, lakini kwa upande wa wachezaji wengine wapo fiti, tunahitaji kushinda mchezo wetu huo,” alisema Djuma.

Tupe Maoni Yako