Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

George Lwandamina Azuiwa Zambia Kisa....


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, amezuiwa nchini kwao Zambia baada ya kuugua ghafla, hali itakayomfanya kuchelewa kurejea nchini kuendelea na majukumu yake.
Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema Lwandamina ilikuwa arejee nchini Jumatatu, lakini kutokana na maradhi aliyoyapata, amelazimika kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kabla ya kuruhusiwa kusafiri.
“Kocha tangu alipofika Zambia alipatwa na homa ya malaria akawekwa mapumziko kwa ajili ya kuangalia afya yake kwa ukaribu zaidi, lakini leo (jana) au kesho (leo), atarejea hapa nchini,” alisema Saleh.

Tupe Maoni Yako