Saturday, January 6, 2018

Mawingu Tz

Ishu Ya Okwi Kugoma Kurejea Kisa Kuwadai Simba,Simba Wafunguka Haya

ISHU YA OKWI KUGOMA KUREJEA KISA KUWADAI SIMBA,SIMBA WAFUNGUKA HAYA
Klabu ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imekanusha vikali taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya Habari kuwa klabu hiyo imeshindwa kuwalipa fedha za usajili baadhi ya wachezaji wake.
Baadhi ya vyombo vya habari vimewataja wachezaji hao kuwa ni Emmanuel Okwi na Asante kwasi kuwa hawatacheza hadi walipwe fedha zao za usajili, jambo ambalo Simba imesema si la kweli.
Simba imesema taarifa hizo zimejikita kwenye kuharibu taswira ya klabu, na yenye nia ovu kwa timu ya Simba ambayo ipo kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea huko Zanzibar kwa sasa.
-Simba inapenda kuwaambia wanachama na washabiki wake kuwa, haidaiwi na mchezaji yoyote pesa yoyote si tu ya usajili hata za mishahara,” imesema taarifa hiyo.
Okwi ataonekana hivi karibuni.
-Tupende pia kuwaarifu mchezaji Emmanuel Okwi ataonekana uwanjani hivi karibuni baada ya ruhusa yake ya matibabu kumalizika, huku Kwasi akiendelea kuitumikia klabu kama mlivyoona kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri toka kisiwani Pemba,” Ilisema taarifa hiyo iliyoandikwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara.
Ikumbukwe mlinzi Asante Kwasi alikuwapo kwenye kikosi kilichocheza na Jamhuri ya Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi na kufanikiwa kufunga bao la tatu katika ushindi wa mabao 3-1.

Tupe Maoni Yako