Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

MkudeTshabalala,Mzamiru Haooo SAUZI


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania aliyesajiliwa na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini, Elias Maguli, amewataka wachezaji wengine wachangamkie fursa ya kucheza soka la kulipwa.
Maguli aliyewahi kucheza katika timu za Simba, Stand United na Ruvu Shooting, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Polokwane City baada ya kuachana na klabu ya Dhofar ya nchini Oman.
Akizungumza na Chandimu  jana, Maguli alisema hapa nchini kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka la kulipwa lakini wanashindwa kuchangamkia fursa hiyo.
Aliwataja baadhi ya wachezaji ambao viwango vyao vinawaruhusu kucheza soka la kulipwa kuwa ni Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Rafael Daudi, Mzamiru Yassin na Rajab Zahir.
Alisema wachezaji hao wanatakiwa kupambana na kuikabili changamoto ya kukatishwa tamaa ili kufikia malengo yao, viwango walivyonavyo havina tofauti na wale anaokutana nao katika klabu za nje.
“Tanzania kuna wachezaji wengi ambao wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa, kinachowakwamisha ni kudharauliana wenyewe kwa wenyewe na kukatishana tamaa,” alisema Maguli.
Tetesi za awali zilidai kuwa straika huyo alikuwa na mpango wa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Simba pamoja na Yanga katika dirisha dogo la usajili, lakini mambo yakaenda tofauti.

Tupe Maoni Yako