Tuesday, December 12, 2017

Mawingu Tz

Haya Hapa Makundi Kombe La Mapinduzi...Singida UTD Yaongezwa...Mtibwa OUT

MPYA : Makundi kombe la Mapinduzi 2017
Makundi kombe la Mapinduzi 2017 leo yametangazwa huku Simba na Azam wakijikuta kwenye Kundi Moja na Wageni Waalikwa URA kutoka NCHINI Uganda.
Katika Kundi A Kuna Timu za Azam Fc (Mabingwa watetezi) , Jamhuri , Mwenge, Simba Na URA kutoka Uganda.
Kundi B Lina timu za Yanga, JKU, Mlandege Fc. Singida United, Taifa Jang’ombe na Zimamoto.
Kamati itakutana kupanga ratiba kamili na leo ilikuwa siku ya Kutangaza Makundi tu
“Tunataraji kutoa ratiba rasmi ya mashindano hayo hivi karibuni, kwani hivi sasa tunakamilisha hatua za mwisho ambapo kina jambo dogo tu limejitokoeza ndio maana tumechelewa ila ratiba itatoka mapema,”
Alisema baada ya Kutangaza makundi hayo moja kati ya wajumbe wa kamati ya Mashindano hayo, Kama kawaida kwataunit.com tutakuwa nawe sambamba kukupa kila linalohusu Mashindano haya.


Tupe Maoni Yako